Tue, November 29, 2022

The Revolutionary Government of Zanzibar

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Zanzibar Dr. Othman Abbas Ali akikabidhi Ripoti za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali Zanzibar Dr. Othman Abbas Ali akikabidhi kwa Mhe. Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi  Ripoti za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Ripoti hizo ni za aina sita (6) ambazo ni Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Mawizara, Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Mashirika, Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Mitaa, Ripoti ya Ukaguzi wa Mifumo ya Tehama, Ripoti ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo pamoja na Ripoti ya Ukaguzi Maalum ambapo ghafla hiyo ilifanyika Siku ya Jumamosi tarehe 27 Agosti 2022 IKULU – Zanzibar.