TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Wazanzibari wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi nne (4) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984, Kifungu 112 kwa lengo la kudhibiti na kukagua Hesabu za Serikali na kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya Rasilimali za Umma ambazo zimeidhinishwa na Baraza la Wawakilishi kwa mujibu wa Sheria.
NAFASI ZA AJIRA
Mkaguzi wa Kiuchunguzi (Forensic Auditor) Daraja La II – Nafasi 4 Unguja.
MAJUKUMU YA KAZI
- Kufanya ukaguzi na uchunguzi wa Mifumo ya TEHAMA endapo kutakuwa na uhalifu au makosa ya kimfumo ambayo yametendeka.
- Kukusanya ushahidi wa kiuchunguzi ikiwa Mifumo ya TEHAMA itatumika kinyume na utaratibu.
- Kuandaa Ripoti ya Ukaguzi wa uchunguzi uliofanyika.
- Kuandaa miongozo ya ukusanyaji ushahidi wa kiuchunguzi.
- Kufanya Uchambuzi wa taarifa za kiuchunguzi kwa kutumia zana za TEHAMA.
- Kufanya Tafiti mbali mbali zinazohusiana na ukaguzi wa kiuchunguzi.
- Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake wa kazi zinazoendana na sifa na fani yake.
2
SIFA ZA MWOMBAJI - Muombaji awe Mzanzibari na mwenye umri usiozidi miaka 40.
- Muombaji awe na elimu ya Shahada ya kwanza/ Stashahada ya Juu katika fani zifuatazo:-
Uhasibu wa Kiuchunguzi (Forensic Accounting/Finance).
Usalama wa Kimtandao (Network / Cyber Security)
Usalama wa Taarifa (Information Security)
Sayansi ya Kompyuta (Computer Science)
Sayansi ya Data (Data Science)
Uchambuzi wa Data (Data analytics)
Uhandisi wa Taarifa (Information Engineering)
Fani nyengine inayofanana na hizo. - Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini.
SIFA ZA ZIADA
Awe amethibitishwa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (Certified Public Accountant).
Awe mkaguzi wa mifumo ya TEHAMA aliyethibitishwa na Taasisi zinazotambulika (Certified Information System Auditor).
Awe amethibitishwa kufanya ukaguzi wa kiuchunguzi (Certified Forensic Investigator).
Awe na Cheti cha Sheria kutoka katika Chuo kinachotambulika na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MSHAHARA
Mtumishi atalipwa kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; Ngazi ya mshahara ZPSG-09.
3
MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI
Barua za maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
i. Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
ii. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo na kwa aliyesoma nje ya Tanzania anatakiwa kuambatanisha kivuli cha cheti cha uthibitisho kutoka TCU.
iii. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
iv. Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.
v. Picha ya rangi ya muombaji ya karibuni (Current Colored Passport Size Picture).
MUHIMU:
Vivuli vya vyeti vya muombaji vithibitishwe na Mamlaka husika (Certified Copies).
Maombi yote yatumwe kwa kutumia baruapepe application@ocagz_.go.tz na yaelekezwe kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
S.L.P 258 Maisara – Zanzibar.
Kwa muombaji yoyote atakaewasilisha “Provisional result, Statement of result, Progressive reports” au kuwasilisha maombi yake kwa njia nyengine yoyote isiyokuwa ya baruapepe maombi yake hayatozingatiwa.
Mwisho wa kupokea maombi haya ni tarehe 16/06/2023.
Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Ofisi: www.ocagz_.go.tz