Tangazo la nafasi za Kazi
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984, Kifungu 112 kwa lengo la kudhibiti na kukagua Hesabu za Serikali na kuhakikisha kwamba kunakuwa na uwajibikaji na uwazi katika matumizi ya fedha na usimamizi wa Rasilimali za Umma.
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inatangaza nafasi za kazi kwa
waombaji wenye sifa na uwezo kama ifuatavyo:-
1.0 MKAGUZI WA HESABU DARAJA LA II (AUDITOR GRADE II) – NAFASI 1 UNGUJA
1.1 Majukumu ya Kazi
i. Kufanya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa Mawizara, Mashirika, Wakala, Mamlaka
pamoja na Miradi ya Maendeleo;
ii. Kufanya utekelezaji wa mpango kazi wa ukaguzi wa kila mwaka;
iii. Kufanya ufuatiliaji wa hoja za ukaguzi zinazotolewa baada ya ukaguzi kukamilika;
iv. Kuandaa ripoti za ukaguzi kwa wakati.
v. Kutunza na kuweka kumbukumbu mbalimbali za kazi za ukaguzi katika eneo lake la
kazi; na
vi. Kufanya kazi nyingine zozote zinazohusiana na kada yake atakazopangiwa na mkuu
wake.
1.2 Sifa za Muombaji
- Awe ni Mzanzibari mwenye umri usiozidi miaka 46.
- Awe na elimu ya Shahada ya kwanza/Stashahada ya Juu ya Uhasibu au fani inayofanana kutoka Vyuo Vikuu au Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta kwenye kuandika na kufanya mahesabu.
1.3 Sifa za Ziada
Waombaji wenye ujuzi na sifa zifuatazo watapewa kipaumbele:
- CPA (Certified Public Accountant)
- Kutumia programu za Uhasibu na Ukaguzi (ACL, IDEA, Team Mate, etc)
- Uzoefu katika kazi za Uhasibu, Ukaguzi au usimamizi wa fedha.
1.4 Mshahara
Mtumishi atalipwa kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar; Ngazi ya mshahara ZPSJ-01.
1.5 Masharti ya Jumla kwa Waombaji
Barua za maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:
i. Maelezo binafsi ya muombaji (CV).
ii. Vivuli vya vyeti vya kumalizia masomo, kwa waliosoma nje ya Tanzania wanatakiwa
kuambatanisha vyeti vyao vya uthibitisho kutoka TCU.
iii. Kivuli cha cheti cha kuzaliwa.
iv. Kivuli cha kitambulisho cha Mzanzibar mkaazi.
v. Picha ya muombaji ya karibuni (Colored Passport size).
MUHIMU:
- Maombi yote yawasilishwe kwa njia ya Kielektroniki kwenye Mfumo wa Ajira wa Serikali (ZanAjira) kupitia anuani ifuatayo https://portal.zanajira.go.tz
- Mwisho wa kupokelewa maombi hayo ni tarehe 12 Septemba, 2025.
- Vivuli vya vyeti vya muombaji vithibitishwe na Mamlaka husika (Certified Copies).
- Maombi yote yaelekezwe kwa anuani ifuatayo:
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
Afisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali,
S.L.P 258, Maisara – Zanzibar.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia nambari 0773 258884 au nambari
0776 677516. Vile vile unaweza kutembelea tovuti ya Ofisi kwa taarifa zaidi:
www.ocagz.go.tz